Botswana yaipatia Zimbabwe dola milioni 600
27 Februari 2019Botswana ambayo ina utajiri mkubwa wa madini ya Almasi imesema itaipatia Zimbabwe karibu dola milioni 600 kuisaidia nchi hiyo kupunguza mzozo wake wa kiuchumi, gazeti la serikali la Zimbabwe The Herald limeripoti.
Mkopo huo utatolewa katika sekta ya binafsi nchini Zimbabwe pamoja na sekta ya machimbo ya almasi, ripoti hiyo imesema. Waziri wa mambo ya kigeni wa Zimbabwe James Manzou , amefichua pendekezo hilo kabla ya ziara mjini Harare itakayofanywa na rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi.
Zimbabwe ilitumbukia katika hali mbaya ya kiuchumi katika miaka 37 ya utawala wa rais Robert Mugabe ambaye alilazimishwa kuondoka madarakani mwaka 2017.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Zimbabwe amesema nchi yake inakaribisha pendeekezo hilo la Botswana na kwamba mkopo huo utasaidia ufufuaji wa uchumi wa nchi hiyo.