Kansela Olaf Scholz ashinikizwa kutowania tena ukansela
18 Novemba 2024Chama hicho badala yake kinamtaka asafishe njia kwa Waziri wa Ulinzi Boris Pistorius kupitia chama hicho cha Social Democrats (SPD) katika uchaguzi mkuu ujao.
Joe Weingarten na Johannes Arlt, ndio wabunge wa kwanza wa SPD kumpigia debe Pistorius ambaye ni maarufu zaidi kuliko Scholz, kulingana na kura za maoni.
Mnamo mwezi Julai, Scholz alitangaza nia yake ya kuwania tena ukansela, miezi kadhaa kabla ya kuporomoka kwa serikali ya mesto wiki iliyopita.
Kufuatia kuporomoka kwa serikali inayoongozwa na Scholz, kura ya Imani imeshapangwa na uchaguzi wa mapema vilevile unatarajiwa kufanyika Februari badala ya Septemba.
Hata hivyo Scholz amesimama kidete na mpango wake akisema yeye na chama cha SPD wako tayari kwa michakato hiyo kw alengo la kushinda.