Chama cha Kijani cha Ujerumani kimechagua mwenyekiti mwenza
16 Novemba 2024Banaszak alipata asilimia 92.88 ya kura, akipata nafasi ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka miwili.
Brantner alichaguliwa kuwa mwenyekiti mwenza mwingine wa chama hicho kwa asilimia 78.15 ya kura, na amekuwa mwanachama wa Bundestag ya Ujerumani tangu uchaguzi wa kitaifa wa 2021.
Soma pia: Serikali ya Ujerumani yasambaratika kutokana na uchumi unaoyumba
Akizungumza baada ya kuchaguliwa kwake Brantner amesema Ujerumani inahitaji uwekezaji zaidi, huku kukiwa na wasiwasi kuhusu uchumi wa taifa.
Katika mkutano huo wa siku mbili, chama cha Kijani pia kinatarajiwa kukubaliana iwapo Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Robert Habeck, kuwa mgombea wake wa ukansela katika uchaguzi ujao.
Soma pia: Viongozi wa Chama cha Kijani Ujerumani waamua kuachia ngazi
Ujerumani inajiandaa kwa uchaguzi wa mapema, unaotarajiwa Februari, kufuatia kuanguka kwa muungano wa serikali wiki iliyopita.