Chama cha upinzani nchini Angola kimekataa matokeo ya uchaguzi wa rais ambao ulikipa ushindi chama tawala cha MPLA wa asilimia 51.17, huku UNITA ikija katika nafasi ya pili kwa asilimia 43.95. UNITA kimetoa hoja ya kwamba tume ya uchaguzi haikukishirikisha ipasavyo katika hatua za mwisho za kuidhinisha matokeo. Daniel Gakuba amezungumza na Francis Mndolwa, balozi mstaafu nchini Tanzania.