COP 29 yaingia katika siku ya ziada Azerbaijan
23 Novemba 2024Matangazo
Katika jitihada ya kupata ahadi bora za uchangiaji wa fedha kwa mataifa yaliondelea kwa ajili kukabiliana na athari za kimazingira. Rasimu ya makubaliano ya mwisho ya Jana Ijumaa ilionesha ahadi ya dola bilioni 250 kila mwaka hadi ifikapo 2035, ikiwa ni zaidi ya mara mbili ya lengo la awali la dola bilioni 100 lililowekwamiaka 15 iliyopita, kiwango ambacho pia wataalamu walisema kina upungufu wa zaidi ya dola trilioni moja kwa makadirio ya uhitajii Katika nyakati za mapema za Asubuhi ya leo shirika la habari la The Associated Press liliwashuhudia wapatanishi wakuu kutoka Umoja wa Ulaya, Marekani na mataifa mengine katika maeneo ya kumbi kadhaa kwa lengo la kufanya mikutano ya kujaribu kuharakisha makubaliano mapya ya mpango huo.