Dakta Abdalla Possi "Ulemavu si Kilema"
31 Machi 2015Matangazo
Ama kweli "Ulemavu si Kilema". Huu ni msemo ambao umetimia kwa Dakta Abdallah Possi, mlemavu wa ngozi nchini Tanzania. Kwa bidii kubwa aliyoifanya maishani, na bila kujali changamoto zilizomkabili katika jamii, amesomea uanasheria na kufaulu kujiendeleza katika taaluma hiyo kufikia kuwa mhadhiri wa masuala ya sheria katika chuo kikuu cha Dodoma. Kifupi yeye amebobea katika taaluma hiyo, licha ya kwamba ni mlemavu wa ngozi.
Kukisikiliza kipindi bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi:Josephat Charo
Mhariri:Daniel Gakuba