EU yazionya nchi zake zijiandae kwa wimbi la homa ya nyani
16 Agosti 2024Matangazo
Hii ni baada ya Sweden kutangaza mgonjwa wa kwanza mwenye virusi vya homa ya nyani.
Kituo cha Ulaya cha kuzuia na kudhibiti magonjwa ECDC kimesema hali ya hatari ndani ya Umoja wa Ulaya bado iko chini.
Kituo hicho hata hivyo kimetoa mwito kwa mamlaka za afya umma ndani ya Umoja huo kuwa macho na kuuhamasisha umma juu ya ugonjwa huo.
Mkurugenzi wa kituo hicho cha ECDC Pamela Rendi-Wagner amesema katika taarifa kuwa, Ulaya inapaswa kujiandaa kwa wagonjwa zaidi hasa aina mpya ya virusi vya homa ya nyani vya clade 1.