MigogoroIsrael
Yoav Gallant aunga mkono kuachiliwa mateka
10 Septemba 2024Matangazo
Gallant ameongeza kuwa makubaliano hayo yataipatia Israel, fursa ya kimkakati ya kushughulkia masuala mengine ya kiusalama.
Akizungumza na waandishi wa habari wa kigeni, waziri huyo wa ulinzi amesema suala la kuwarejesha nyumbani mateka ndio jambo sahihi la kufanya.
Ameitolea mwito jumuiya ya kimataifa kuendelea kuishinikiza Hamas kufikia makubaliano, na kuunga mkono kwa dhati hatua ya kwanza ya makubaliano ya awamu tatu ya kusitisha mapigano yaliyotangazwa na Rais wa Marekani Joe Biden mnamo Mei 31.
Wakati huohuo wizara ya afya ya Gaza inayoongozwa na Hamas, imesema hadi kufikia sasa watu waliouawa katika mapigano imefikia watu 41,020.